Monday, June 17, 2024
spot_img
HomeKenya NewsMAKOVU YASIOFUTIKA : Kijiji cha watu walemavu Bungoma

MAKOVU YASIOFUTIKA : Kijiji cha watu walemavu Bungoma

Kijiji cha Bisunu  kimesongwa na umelemavu wa kila nui si vipofu, si chongo, si gumba, viziwi si punguani na hata viwete. Kando na kijiji hiki cha ajabu kusongwa na ulemavu wa kila aina, kimesongwa na uchochole wa kupigiwa mfano.

Na Seliphar Musungu, KAKAMEGA  

Siku zote mwiba wa kujidunga hauna pole na majuto ni mjukuu huja kinyume. Usemi huu unatupeleka moja kwa moja katika kijiji cha Bisumu, gatuzi la Bungoma ambapo wakaazi wa kijiji hicho wanasimulia tukio lililotokea miaka mingi iliyopita na kusababisha madhara na makovu ya milele kwa wakaazi wa kijiji hicho.

Makovu haya yalianza pale ambapo mtu mmoja kutoka katika kijiji hiki alitendewa unyama hadi kuuwawa na wakaazi wa kijiji hiki. Kila boma lina mwana aliye na matatizo ya kimaumbile ambapo wengine ni vipofu, wengine wamezaliwa bila viungo vyote vya mwili kama vile mikono na hata miguu. Maajabu haya.

Bi Agnes Nasipwondi, mama ya watoto watatu na wajukuu wawili vipofu

Kweli kutembea kwingi ndiko kuona mengi na ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni, nilifanya uamuzi wa kukitembelea kjiji hiki cha ajabu ndiposa niweze kuona maana kuona ni kuamini. Kwa umbali nilikiona kijiji cha Bisumu, kilikuwa sawa na vijiji vingine katika jimbo hilo. Kwa makini nilikisogelea kijiji hicho, nilifahamu kwamba kina upekee usio wa kawaida. Upekee unaoashiria kwamba kina mengi ya kusimulia.

Kijiji cha Bisunu  kimesongwa na umelemavu wa kila nui si vipofu, si chongo, si gumba, viziwi si punguani na hata viwete. Kando na kijiji hiki cha ajabu kusongwa na ulemavu wa kila aina, kimesongwa na uchochole wa kupigiwa mfano.

Kwa sababu ya unyanyapaa na ufudhuli huu Milton alifanya uamuzi wa kumchumbia jirani yake, Pamela Nekesa ambaye pia hana uwezo wa kuona. Walijaliwa mtoto wa kike wakampa jina Marion na ambaye alikuwa kipofu siku chache baada ya kuzaliwa.

Milton Wafula (katikati) na nduguzake vipofu

Kulingana na maelezo niliyopewa, wakati mwingine wenyeji hushinda siku nzima bila kutia chochote mdomoni. Kwa kutaka kujua zaidi nilipata fursa ya kuuliza chanzo cha masaibu hayo.

Nilikutana na mzee kwa jina Fred Kasimoto ambaye ni mkaazi wa kijiji hiki na anaufahau zaidi wa masaibu yanayokumba kijiji hiki. Kasimoto alinieleza kwamba wakaazi wa kijiji hicho walimtendea unyama na kumuua mtu mmoja aliyekuwa amemchumbia msichana kutoka katika kijiji hicho na alikuwa na ulemavu.

Hillary, mjuu wa Agnes Nasipwondi ambaye hana uwezo wa kuona

Kifo cha huyo mtu ambaye kulingana na wenyeji wa bisumu hawakumuona kama mtu anayeweza kumchumbia msichana yeyote katika kijiji hicho kwa sababu ya ulemavu wake. Alieleza kwamba zaidi ya majumba 27 yamesongwa na magonjwa mbalimbali yasiyokuwa na tiba.

Kati ya familia  ambazo zimeadhirika familia iliyoadhirika zaidi ni ile ya mama Agnes Nasipwondi. Mama huyu alijaliwa watoto wanane ambapo kati  yao kuna watoto wakiume wanne na wa kike wane. Kwa bahati mbaya mmoja wa watoto wa kike ni marehemu.

Kwa bahati nzuri nilipata fursa ya kuzungumza na Agnes aliyenisimulia hadithi ya maisha yake na wanawe vipofu. Huku amejishika tama na kwa sauti ya upole na yenye  huzuni alieleza kwamba wana wake wote ni vipofu na kila juhudi za kuwataftia matibabu ziliambulia patupu kwani hakuna hasipotali iliyokuwa na suluhu kwa wanawe. 

Agness alikata tama na kukubali kuishi na wanawe jinsi walivyo maana lisilo na budi hutendwa. Mama hamtupi mwanawe, Agness alishi na wanawe mpaka pale wale wa kike waliweza kupata jiko. La kustajabisha ni kwamba laana hii iliwafuata wanawe hadi kule walikoolewa ambapo walijifungua watoto wasio na uwezo wa kuona. Kwa sabau ya kujifungua watoto vipofu wana wake wa kike walipewa talaka na kurudi nyumbani.

Aibu, fedheha na taabu walizopitia katika ndoa zao kwa sababu ya kujifungua wana vipofu mmoja wa wototo wa Agnes aliapa kutooleka tena ili ujiepusha na unyanyapaa huo.

Milton Wafula ni mwana wan ne wa Agnes ambaye kulingana na ufafanuzi wake alizaliwa na kisha kupoteza uwezo wa kuona baada ya siku tatu. Nyota ya jaha ilimuonekania Milton.  Alijaliwa kumpata mhisani aliyefadhili masomo yake hadi pale alipohitimu kuwa mwalimu.

Milton amepitia mengi maana maisha yake hayajawa mteremko, yalikumbwa na panda shuka nyingi. Haikuwa rahisi kwake yeye kutangamana na wenzake. Wengi walimuona kama mtu nasiyefaa.  Hata pale alipotafuta ajira hakuna aliyetaka kumuajiri sababu yeye kipofu. Hakuna aliyeangalia ujuzi wake, maumbile yake yalizungumza zaidi.

Kwa sababu ya unyanyapaa na ufudhuli huu Milton alifanya uamuzi wa kumchumbia jirani yake, Pamela Nekesa ambaye pia hana uwezo wa kuona. Walijaliwa mtoto wa kike wakampa jina Marion na ambaye alikuwa kipofu siku chache baada ya kuzaliwa.

 Katika familia hii ya Agness nakutana na mjukuu wake ambaye alipoteza uwezo wa kuona siku chache baada ya kuzaliwa. Hilary mwenye umri wa miaka 12 na yuko katika darasa la tano.

Nikiachana na familia ya Agness nakutana na Betty Jeruto, wa miaka 32, kwake mambo ni tifauti kidogo. Kwake si vipofu.  Jeruto anasema kwamba mwanawe wa miaka mitano alizaliwa bila mikono na anatumia miguu kuandika.

Hayo ndio maajabu niliyoyashuhudia katika kijiji hiki cha ajabu. Je kwako wewe hii ni laana ama ni genetiki?

Mwisho

RELATED ARTICLES

Most Popular

Recent Comments