Seliphar Musungu
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 23 anauguza majeraha mabaya ya moto na ya kupigwa mwilini mwake katika mtaa wa Mulunyu mjini Kakamega.
Gentrix Kahela Njoroge alichomwa na maji moto na kupigwa kitutu na mumewe wa miezi saba. Unyama huo ukimwacha Gentirx na vidonda vikubwa.
Alielezea kwamba chanzo cha haya yote ni baada ya kuamua kukatisha uhusiano wake na mumewe baada ya kugundua kwamba mumeweana mke mwingine.
“Niliamua kuondoka kurudi nyumbani baada ya kwenda muda mchache alinifuata kwa pikipiki na kuanza kunipiga njiani baadaye akanirudisha kwa nyumba aliponitendea unyama huu.” Gentrix aeleza.
Gentrix alisema kwamba baada ya kupigwa na kuchomwa mumewe alimfungia chumbani hata asipate nafasi ya kwenda haja.
Gentrix hakupata matibabu yoyote na baada ya wiki moja mumewe alimsafirisha hadi kapenguria anakokaa dadake likini dadake alikataa na gentrix kurudishwa kakamega.
“Baada ya wiki moja alinipeleka kwa dadake kapenguria lakini dadake alikataa akihofia kwamba nangefariki wakati wowote kutokana na hali yangu. Alinirudisha nyumbani nilipomwambia kwamba nataka kurudi kwetu alisema kwamba ataleta dakitari anipe matibbau ya nyumbani.” Gentrix asema
Familia yake Gentirx imeghadhabishwa na kitendo hicho na kuomba serikali kuingilia kati ili mshukiwa huyo aweze kutiwa mbaroni.
Kulingana na nyanya yake gentrix hii sio mara ya kwanza mumewe Gentrix amemtendea mnyama huo. Anasema kwamba mwaka jana mumewe Gentrix alimpiga na akarejea nyumbani.
“Tangu mwaka uliopita mwezi wa nane alipoondoka hapa nyumbani sisi kama familia tunamuona leo tena kama amejeruhiwa vibaya zaidi ukilinganisha na mara ya kwanza.” Nyanya yake Gentrix asimulia
Mama yake kwa upande mwingine anadokeza kuwa uhusiano wa mwanawe na mumewe haujakuwa wa manufaa kwa manawe maana amekuwa akidhulimiwa na kuumizwa sana. Mamake pia alieleza kwamba tangu mwanawe arudishwe nyumbani hajapata matibabu maana hawana pesa za matibabu.
Familia hiyo inaomba serikali kufanya uchunguzi ili wanao tenda unyama huu waweze kutiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka ili kuwanusuru wale wote wanaopitia hali ya unyanyasaji wa aina hii.
Mwisho