Kakamega
Collins Chibole na James Boaz Eshitemi
Kifo cha Prof Ken Waliaula walibora huenda ndilo pigo kubwa Zaidi kuwaikutokea kwa ulingo wa Kiswahili na waenzi wa kazi zake.Hadi kifo chake,Ken Walibora amekuwa mlezi wa wengi katika ulimwengu wa kiswahili.
Kando na waandishi, walimu na wahadhiri wengi ambao walikikumbatia Kiswahili katika maandishi, Walibora aliichangamkia lugha ya Kiswahili pia katika baghwabaghwa za kila siku hususan kama mwanahabari na pia kupitia kampeni za kuimarisha lugha ya Kiswahili.
Tuzo tatu mtawalia alizopokea za Jomo Kenyatta literature prize kufuatia vitabu vyake, Ndoto ya Amerika, Kisasi Hapana na Nasikia Sauti ya Mama, zinapeana taswira ya mwandishi aliyeumiliki ulimwengu fulani katika uandishi wa lugha. Marehemu amejipatia sifa kutokana na uandishi wake uliokosha wengi, uchapishaji na uhariri vyote ambavyo alifanya kwingi ikiwa ni pamoja na Kidagaa Kimemwozea
Siku Njema, Ndoto ya Amerika,Kisasi Hapana, Nasikia Sauti ya Mama,Damu Nyeusi, Nizikeni Papa Hapa miongoni mwa nyingine.
JAMES BOAZ ESHITEMI
Japo kwa wengi yaonekana habari ila kwangu itasalia jinamizi manake yanikwepa maneno mahususi ya kumrejelea shujaa, jagina na gwiji ‘mungu’ wa waswahili Ken Waliaula almaarufu Walibora .
Mwaka wa 2005 nikiwa shule ya msingi ya Eshiakhulo wilayani Mumias kaunti ya Kakamega ndipo ilikuwa kaski yangu ya kwanza kusikiza habari, mawazo na ulumbi wa mwandishi huyu mahiri kupitia kwa vitabu alivyoandika.
Riwaya ya Siku Njema ,Ndoto ya Almasi na Kufa Kuzikana ni miongoni tu mwa gange zake zilizonivutia katika shule ya msingi kutokana na jinsi alivyozichambua mwalimu Lina Akacha, kabla ya kujiunga na shule ya upili ya Lubinu nilikokutana na bwana Odali Victor aliyenipa motisha ya kuendeleza kukisoma kiswahili na hata kukizungumza.
Japo kwa mukhtasari kutokana na kazi yake Ken Walibora nimeweza kufunza lugha pana ya kiswahili, kufanya katika vituo kadha vya utangazaji,kando na kuwa mhutubu katika makongamano anuwai hapa nchini kenya.
Baadaye nilijiunga na chuo kikuu cha Masinde Muliro kama mwalimu wa lugha ya kiswahili tokea mwaka wa 2013 nilikoichangamkia lugha hii aula ya Kiswahili. Japo kwa athari za lugha mame mara nyingi tulijifunga kibwebwe na kusaliti mila zetu kwa kuiasi lugha mame. Kiswahili kiliniezesha kuisatili jamaa yangu kwa kuienzi kazi yake.
Japo kwa mukhtasari kutokana na kazi yake Ken Walibora nimeweza kufunza lugha pana ya kiswahili, kufanya katika vituo kadha vya utangazaji,kando na kuwa mhutubu katika makongamano anuwai hapa nchini kenya. Japo kwa kumbukizi zake Ken Walibora ni kwamba mti mkuu umeanguka ila viziki vingali na rotuba linapochomoza shamzi kwa wengi huwafikia mwangaza ila kwa wachache huwafaidi. Kwa wengi hunyaa mvua ila kwa wachache huipata mbegu ya kutia arthini.
Amewalea wanahabari chipukizi kando na kuvipalilia vipaji chipukizi katika Nyanja za Kiswahili. Itakumbukwa kuwa Prof Ken Walibora amekuwa kielelezo kwa waandishi wenzake, wanahabari, Na hata walimu kwa ujumla bila kuwasaza waenzi asharafu wa lugha pana ya Kiswahili na tanzu zake.
Prof Ken Walibora amekuwa nguzo muhimu katika tasnia nzima ya Kiswahili na wapenzi wake. Ina maana Walibora amekuwa ‘mungu’ wa waswahili.
Amewalea wanahabari chipukizi kando na kuvipalilia vipaji chipukizi katika Nyanja za Kiswahili. Itakumbukwa kuwa Prof Ken Walibora amekuwa kielelezo kwa waandishi wenzake, wanahabari, Na hata walimu kwa ujumla bila kuwasaza waenzi asharafu wa lugha pana ya Kiswahili na tanzu zake.
Tangia lugha ya Kiswahili kufanywa linkua franka nchini kenya Prof Ken Walibora amekuwa mstari wa mbele katika kukilonga Kiswahili haswa katika miktadha tofauti tofauti ikiwemo makongamano, katika vyuo vikuu,taasisi mbalimbali ikiwemo shule za upili na zile za msingi.
Lugha aliyoitumia mwandishi Ken Walibora katika kazi zake ilikuwa lugha ya kipekee iliyosheheni ufundi wa kipekee. Ken Walibora pia ameichora taswira ya matabaka mawili; tabaka la wakwasi na lile la walalahoi.
Walibora alitoa mtafaruku uliopo katika uongozi kando na kuichora picha kamili inayojitokeza wazi kati ya walio na kisomo bila ajira na wenye ajira bila kisomo katika ukinzani. Kwa kauli yangu, mwandishi Ken Walibora licha ya kututangulia mbele ya haki atasalia katika nyoyo zetu kama waenzi wa lugha ya Kiswahili kutokana na vile alivyokua na ufundi wa namna yake katika tasnia nzima ya Kiswahili.
Mchango wako utatulazimu tukuite hayati. Nani anakujua ni msamiati ambao umekula wengi na hata kuwaelekeza wengi wa adinasi ahera. Siku zote umesema chema hakidumu … uru Ken Walibora safiri salama mfahamishe JALALI KUWA CHINI WINGU NI SAMAWATI KWA KULITAZAMA.
COLLINS CHIBOLE
Nakumbuka nikiwa darasa la nne, babangu aliponitunuku kitabu cha siku njema baada ya kuongoza somo la Kiswahili shule ya msingi ya Eshisenye, ikawa riwaya yangu ya kwanza kuisoma maishani na ukawa mwanzo wa ndoto yangu katika uandishi.
Namtambua Walibora kama aliyechangia pakubwa kufanikiwa kwangu katika lugha ya Kiswahili katika mitihani ya Kitaifa ya KCPE na ya KCSE. Kando na taaluma yangu ya ujasiriamali na fedha, kazi ya walibora ndiyo iliyonisukuma kuandika riwaya yangu ya kwanza ya ‘Nyota ya Mama’ kando na tamthilia ya ‘Fumbo la Imani’.
Walibora ni mwanahabari aliyeumiliki ufundi wa kutamaniwa, mkufunzi na mwandishi aliyeukumbatia ucheshi na ulumbi wa kupigiwa mfano. Si ajabu kwamba , marehemu katika uandishi wake alisisitiza kuwa kila nafsi ni sharti itayaonja mauti, kuna visa si haba vya ubashiri ambavyo vinarejelea kifo chake.
Nilipojiunga na radio MMUST FM mwaka 2013, nilianzisha Makala ya ‘Kisiwa cha Lugha’ na moja kwa moja Walibora akawa mlezi wa Makala hayo licha ya shughuli nyingi zilizomsetiri.
Walibora ni mwanahabari aliyeumiliki ufundi wa kutamaniwa, mkufunzi na mwandishi aliyeukumbatia ucheshi na ulumbi wa kupigiwa mfano. Si ajabu kwamba , marehemu katika uandishi wake alisisitiza kuwa kila nafsi ni sharti itayaonja mauti, kuna visa si haba vya ubashiri ambavyo vinarejelea kifo chake.
Kutoka kwa ufukara, kongowea mswahili mhusika mkuu katika riwaya ya siku njema mwishoni analitazama wingu la magharibi na tabasamu la ufanisi, milki ya babake ikiwa chini yake pamoja na binti Vumilia tamanio la moyo wake.
Kwa mfano katika riwaya ya siku njema, ‘mwili wa Mzee Kazikwisha ulipatikana na mwanawe Msanifu Kombo siku kadhaa baada ya kifo chake. Hakujulikana na wengi kuwa alikuwa Juma Mukosi,msomi wa kutajika, maziko ya juma mukosi yalihudhuriwa na idadi ndogo ya watu’. Mtemi Nasaba Bora katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea alipatikana akiwa ameipa dunia kisogo na mazishi yake kuhudhuriwa na idadi ndogo ya watu. Uandishi wa walibora unasetiri ujumbe wa Tumaini.
Kutoka kwa ufukara, kongowea mswahili mhusika mkuu katika riwaya ya siku njema mwishoni analitazama wingu la magharibi na tabasamu la ufanisi, milki ya babake ikiwa chini yake pamoja na binti Vumilia tamanio la moyo wake.
Mto kiberenge katika riwaya ya Kidagaa kimemwozea, licha ya kuwa ulisetiri laana na kutafsiriwa kuwa hatari kwa yeyote ambaye angeyanywa maji yake, Imani na Amani wahusika wakuu baada ya kuyanywa maji yake walitulizwa kiu na hatimae haki yao kupatikana na mmoja wao kupendekezwa hata kuwa mfalme katika jamii hiyo. Mti mkuu ushavunjika ila kupitia kazi zake, atazaa, atalea, atakuza, ataelimisha na kuhamasisha. Rabi ailaze roho yake mahala pema.
Mwisho.