Kakamega
Collins Chibole na James Boaz Eshitemi
Kifo cha Prof Ken Waliaula walibora huenda ndilo pigo kubwa Zaidi kuwaikutokea kwa ulingo wa Kiswahili na waenzi wa kazi zake.Hadi kifo chake,Ken Walibora amekuwa mlezi wa wengi katika ulimwengu wa kiswahili.
Kando na waandishi, walimu na wahadhiri wengi ambao walikikumbatia Kiswahili katika maandishi, Walibora aliichangamkia lugha ya Kiswahili pia katika baghwabaghwa za kila siku hususan kama mwanahabari na pia kupitia kampeni za kuimarisha lugha ya Kiswahili.

Tuzo tatu mtawalia alizopokea za Jomo Kenyatta literature prize kufuatia vitabu vyake, Ndoto ya Amerika, Kisasi Hapana na Nasikia Sauti ya Mama, zinapeana taswira ya mwandishi aliyeumiliki ulimwengu fulani katika uandishi wa lugha. Marehemu amejipatia sifa kutokana na uandishi wake uliokosha wengi, uchapishaji na uhariri vyote ambavyo alifanya kwingi ikiwa ni pamoja na Kidagaa Kimemwozea
Siku Njema, Ndoto ya Amerika,Kisasi Hapana, Nasikia Sauti ya Mama,Damu Nyeusi, Nizikeni Papa Hapa miongoni mwa nyingine.
JAMES BOAZ ESHITEMI

Japoย kwaย wengiย ย yaonekanaย habari ilaย ย kwanguย itasaliaย jinamiziย ย manakeย yanikwepaย manenoย mahususi yaย kumrejeleaย shujaa, jagina na ย gwijiย โmunguโ waย waswahiliย Kenย Waliaulaย almaarufuย Walibora .
Mwakaย waย 2005 nikiwa shuleย yaย msingiย yaย Eshiakhuloย wilayaniย Mumiasย kauntiย yaย Kakamegaย ndipo ilikuwaย kaskiย yanguย yaย kwanzaย kusikizaย habari, mawazoย naย ulumbiย waย mwandishiย huyuย mahiriย kupitiaย kwaย vitabuย alivyoandika.
Riwaya yaย Siku Njema ,Ndoto ya Almasi naย Kufaย Kuzikanaย niย miongoniย tu mwaย gangeย zakeย zilizonivutiaย katika shuleย ya msingiย kutokanaย naย jinsiย alivyozichambuaย mwalimuย Linaย Akacha, kablaย yaย kujiungaย naย shuleย yaย upili ya Lubinuย nilikokutanaย na ย bwanaย Odaliย Victorย aliyenipa motishaย yaย kuendeleza ย kukisomaย kiswahiliย naย hataย kukizungumza.
Japoย kwaย mukhtasari kutokanaย ย naย kaziย yake Kenย Waliboraย nimewezaย kufunza lughaย pana yaย kiswahili,ย kufanyaย katikaย vituoย kadha vyaย utangazaji,kandoย naย kuwa mhutubuย ย katikaย ย makongamanoย anuwai hapaย nchini kenya.
Baadayeย nilijiungaย naย chuo kikuuย chaย Masindeย Muliro kamaย mwalimuย waย lughaย yaย kiswahili tokeaย mwakaย waย 2013 nilikoichangamkiaย lughaย hii aulaย yaย Kiswahili. Japoย kwaย athariย zaย lughaย mameย maraย nyingiย tulijifungaย ย kibwebweย naย kusalitiย milaย zetuย kwaย kuiasiย lughaย mame.ย Kiswahiliย kiliniezeshaย kuisatiliย jamaa yanguย kwaย kuienziย kazi yake.ย ย

Japoย kwaย mukhtasari kutokanaย ย naย kaziย yake Kenย Waliboraย nimewezaย kufunza lughaย pana yaย kiswahili,ย kufanyaย katikaย vituoย kadha vyaย utangazaji,kandoย naย kuwa mhutubuย ย katikaย ย makongamanoย anuwai hapaย nchini kenya. Japoย kwaย kumbukizi zakeย Kenย Waliboraย niย kwambaย mtiย mkuu umeangukaย ilaย viziki vingali na rotuba linapochomoza shamzi kwa wengi huwafikia mwangaza ila kwa wachache huwafaidi. Kwa wengi hunyaa mvua ila kwa wachache huipata mbegu ya kutia arthini.
Amewaleaย wanahabariย chipukiziย kandoย na kuvipalilia vipaji chipukiziย katikaย Nyanja ย zaย Kiswahili. Itakumbukwaย kuwa Profย Kenย Waliboraย amekuwaย kielelezoย kwaย waandishiย wenzake, wanahabari, Na hataย walimu kwaย ujumlaย bilaย kuwasaza waenziย asharafuย waย lughaย panaย yaย Kiswahili ย naย tanzuย zake.
Prof ย Kenย Waliboraย amekuwaย nguzo muhimu katikaย tasniaย nzimaย ya Kiswahili ย na wapenziย wake. Inaย maana Waliboraย amekuwaย โmunguโย waย waswahili.

Amewaleaย wanahabariย chipukiziย kandoย na kuvipalilia vipaji chipukiziย katikaย Nyanja ย zaย Kiswahili. Itakumbukwaย kuwa Profย Kenย Waliboraย amekuwaย kielelezoย kwaย waandishiย wenzake, wanahabari, Na hataย walimu kwaย ujumlaย bilaย kuwasaza waenziย asharafuย waย lughaย panaย yaย Kiswahili ย naย tanzuย zake.
Tangia ย lughaย yaย Kiswahili ย kufanywaย linkua franka nchiniย kenyaย Profย Kenย Waliboraย amekuwaย mstariย waย mbeleย katikaย kukilongaย Kiswahili ย ย haswa katikaย miktadhaย ย tofauti tofauti ikiwemoย makongamano,ย katikaย vyuoย vikuu,taasisi mbalimbaliย ikiwemoย shuleย zaย upiliย naย zileย zaย msingi.
Lughaย aliyoitumiaย mwandishiย Kenย Waliboraย katikaย kaziย zakeย ilikuwa lughaย yaย kipekeeย iliyosheheniย ufundiย waย kipekee. Ken ย Waliboraย piaย ameichoraย taswiraย yaย matabaka mawili; tabaka la wakwasi naย lileย la ย walalahoi.

Walibora ย alitoaย mtafaruku uliopoย katikaย uongoziย kandoย naย kuichoraย pichaย kamiliย inayojitokezaย waziย katiย yaย walioย naย kisomoย bilaย ajiraย na wenye ajira bila kisomo katika ukinzani.ย Kwaย kauliย yangu, mwandishiย Kenย Waliboraย ย lichaย yaย kututanguliaย mbeleย yaย hakiย atasaliaย katikaย nyoyoย zetuย kamaย waenziย waย lughaย ya Kiswahili kutokana na vile alivyokua naย ufundiย waย namnaย yakeย katikaย tasniaย nzimaย yaย Kiswahili.ย
Mchango ย wakoย utatulazimuย tukuiteย hayati. Nani ย anakujuaย niย msamiatiย ambaoย ย umekulaย wengiย naย hataย kuwaelekezaย wengiย waย adinasiย ahera. Siku ย zoteย umesemaย chemaย hakidumu โฆ uru Ken Walibora safiri salama mfahamishe JALALI KUWAย CHINI WINGU NI SAMAWATIย KWA ย KULITAZAMA.
COLLINS CHIBOLE

Nakumbuka nikiwa darasa la nne, babangu aliponitunuku kitabu cha siku njema baada ya kuongoza somo la Kiswahili shule ya msingi ya Eshisenye, ikawa riwaya yangu ya kwanza kuisoma maishani na ukawa mwanzo wa ndoto yangu katika uandishi.
Namtambua Walibora kama aliyechangia pakubwa kufanikiwa kwangu katika lugha ya Kiswahili katika mitihani ya Kitaifa ya KCPE na ya KCSE. Kando na taaluma yangu ya ujasiriamali na fedha, kazi ya walibora ndiyo iliyonisukuma kuandika riwaya yangu ya kwanza ya โNyota ya Mamaโ kando na tamthilia ya โFumbo la Imaniโ.
Walibora ni mwanahabari aliyeumiliki ufundi wa kutamaniwa, mkufunzi na mwandishi aliyeukumbatia ucheshi na ulumbi wa kupigiwa mfano. Si ajabu kwamba , marehemu katika uandishi wake alisisitiza kuwa kila nafsi ni sharti itayaonja mauti, kuna visa si haba vya ubashiri ambavyo vinarejelea kifo chake.
Nilipojiunga na radio MMUST FM mwaka 2013, nilianzisha Makala ya โKisiwa cha Lughaโ na moja kwa moja Walibora akawa mlezi wa Makala hayo licha ya shughuli nyingi zilizomsetiri.

Walibora ni mwanahabari aliyeumiliki ufundi wa kutamaniwa, mkufunzi na mwandishi aliyeukumbatia ucheshi na ulumbi wa kupigiwa mfano. Si ajabu kwamba , marehemu katika uandishi wake alisisitiza kuwa kila nafsi ni sharti itayaonja mauti, kuna visa si haba vya ubashiri ambavyo vinarejelea kifo chake.
Kutoka kwa ufukara, kongowea mswahili mhusika mkuu katika riwaya ya siku njema mwishoni analitazama wingu la magharibi na tabasamu la ufanisi, milki ya babake ikiwa chini yake pamoja na binti ย Vumilia tamanio la moyo wake.
Kwa mfano katika riwaya ya siku njema, โmwili wa Mzee Kazikwisha ulipatikana na mwanawe Msanifu Kombo siku kadhaa baada ya kifo chake. Hakujulikana na wengi kuwa alikuwa Juma Mukosi,msomi wa kutajika, maziko ya juma mukosi yalihudhuriwa na idadi ndogo ya watuโ. Mtemi Nasaba Bora katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea alipatikana akiwa ameipa dunia kisogo na mazishi yake kuhudhuriwa na idadi ndogo ya watu. Uandishi wa walibora unasetiri ujumbe wa Tumaini.
Kutoka kwa ufukara, kongowea mswahili mhusika mkuu katika riwaya ya siku njema mwishoni analitazama wingu la magharibi na tabasamu la ufanisi, milki ya babake ikiwa chini yake pamoja na binti ย Vumilia tamanio la moyo wake.
Mto kiberenge katika riwaya ya Kidagaa kimemwozea, licha ya kuwa ulisetiri laana na kutafsiriwa kuwa hatari kwa yeyote ambaye angeyanywa maji yake, Imani na Amani wahusika wakuu baada ya kuyanywa maji yake walitulizwa kiu na hatimae haki yao kupatikana na mmoja wao kupendekezwa hata kuwa mfalme katika jamii hiyo. Mti mkuu ushavunjika ila kupitia kazi zake, atazaa, atalea, atakuza, ataelimisha na kuhamasisha. Rabi ailaze roho yake mahala pema.
Mwisho.


