Seliphar, Kakamega
Kila siku, kila uchao visa vya dhuluma dhidi ya watoto vinaongezeka katika kaunti ya Kakamega. Ni kipi kinachosababisha visa hizi? Ni hatua gani inayochukuliwa dhidi ya wale wanaotenda unyama huu? Haya ni baadhi tu ya maswali ambayo kupata majibu yake ni muhali.
Hata hivyo wanaskautiย kutoka katika kaunti ya Kakamegaย wamejitosa uwanjani kukashifu maovu hayo dhidi ya watoto. Wanaskauti haoย wameshiriki matembezi ya amani ya kuwahamasisha wakaaziย kuwa mstari wa mbele katika kuripotiย visa hivyo punde tuย vinapototekea katika jamii.
Matembezi hayo yalingโoa nanga katika eneo bunge la shinyalu ambapo yalihusisha wanafunzi wa shule za msingi wakieneza ujumbe kwa umma wa kukomesha dhuluma dhidi ya watoto.
Sharon Ingato aliyeongoza kikosi hiki alisema kwamba dhulumaย dhidi ya watoto zina madhara mengi kama vile kususia masomo, mimba za mapemaย na hataย sehemu za mwili kuharibika kwa mfano watoto wa kiume wanapo lawitiwa .
โNaomba serikali iweke sheria kali kwa watu watakao patikana kwa makosa yanayohusiana na watoto , pia watoto muwe makini sana mnaporipoti visa hivi maana si kila mtu atakusaidia kupata haki.โย Florence Awinoย adokeza
โKila mtoto ana ndoto yake maishani, tunapowadhulumu hawa watoto tunaua ndoto zao maana kuna wale baada ya kitendo hicho hawatarudi shuleni , kuna mwingine atajitoa uhai. Tumejitokeza ili tupiganie haki za watoto na tukomeshe dhuluma dhidi ya watoto katika kaunti hii.โย Sharon alieleza.
Matembezi haya yaliungwa mkono na baadhi ya walimu katika eneo hilo na kuwasihi watoto kuwa makini wanaporipoti visa kama hivi maana si kila mtu ni mwaminifu na si wote watahakikisha kwamba haki inapatikana.
โNaomba serikali iweke sheria kali kwa watu watakao patikana kwa makosa yanayohusiana na watoto , pia watoto muwe makini sana mnaporipoti visa hivi maana si kila mtu atakusaidia kupata haki.โย Florence Awinoย adokeza
Viongozi wa wanaskauti wameionya jamii dhidi ya kushiriki mazungumzo na kutatua visa vya dhuluma nyumbani, wakisema kuwa kwa mara nyingi wahasiriwa hunyimwa haki
โโWale wanaotekeleza maovu haya wachukuliwe hatua kali ndiposa idadi yaย vitendi hivi iweze kurudi chini. Tunaombaย jamii iwache sheria ichukue mkondo wake, wasiingile kati kwa kutaka kesiย hizi zisuluhishwe nyumbaniย hii ndio sababu kubwa ya kuongezeka kwa dhuluma dhidi ya watoto.โโ Sharon alionya.ย ย
Mwisho


