Biwi la simanzi lilitanda katika kituo kimoja cha Redio cha hapa nchini usiku wa Jumatano baada ya mcheza santuri wao mmoja kuzirai ndani ya studio.
Mcheza santuri Alex Nderi almaarufu DJ Lithium alifariki alipokuwa anapokea matibabu katika hospitali ya Nairobi baada ya kuzirai akiwa ofisini.
Duru za kuaminika zimesema kwamba DJ Lithium aliacha kama ameandika barua na kufuta kurasa zake zote katika mitandao ya kijamii. Baada ya kuona ameanguka, wafanyikazi wenzake walijitahidi kumwamsha bila mafanikio.
Wafanyakazi wenza wamesema wataachia familia ya mwenda zake jukumu la kufungua barua ambayo marehemu aliacha.
Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo. Mkuu wa polisi wa Kilimani Muturi Mbogo amesema Lithium alipelekwa hospitalini kwa ambulans.
"DJ Lithium ajitoa uhai katika ofisi za redio. Aki sisi Wanaume wakati mwingine huwa tunapitia msongo wa mawazo na huwa hatufungukii marafiki kama jinsi wanawake wanavyojadili mambo yao na wanawake wenzao juu asilimia 90 ya maadui wetu ni marafiki wetu" Sonko amesema.
“Alithibitishwa kufariki alipofika,” alisema.
Kisa hicho kilitokea katika Jumba la Lonroh katikati mwa jiji la Nairobi ingawa polisi walifahamishwa baadaye.
Kulingana na mmoja wa wafanyakazi wenzake, DJ huyo alitaja masuala ya kifamilia kuwa miongoni mwa sababu zilizomfanya achukuwe hatua hiyo.
“Alikuwa na maswala ya kifamilia ambayo alitaja kuwa sababu ya tukio hilo. Tumeshtuka,” alisema mmoja wa wafanyakazi hao.
Kisa hiki kilimhuzunisha sana aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko amesema tatizo la msongo wa mawazo ni la kawaida haswa miongoni mwa wanaume na aghalabu huwa hawapatiusaidizi kwa muda ufaao kwani wengi wao hupendelea kusalia kimya na kupambana na hali yao kivyao.
“DJ Lithium ajitoa uhai katika ofisi za redio. Aki sisi Wanaume wakati mwingine huwa tunapitia msongo wa mawazo na huwa hatufungukii marafiki kama jinsi wanawake wanavyojadili mambo yao na wanawake wenzao juu asilimia 90 ya maadui wetu ni marafiki wetu” Sonko amesema.
Ends