Friday, December 27, 2024
spot_img
HomeKenya NewsJe! Fernandes Barasa ana suluhu?

Je! Fernandes Barasa ana suluhu?

Na Collins Matubwi

Nairobi

Ni bayana bikuli kuwa asilimia kubwa ya wanasiasa kutoka gatuzi la kakamega wamehusishwa angalau kwa hatua fulani na kuangamia kwa kampuni ya sukari ya Mumias hususan walio kipaumbele kuzungumzia mdahalo tata wa mhisani kumkabidhi mwekezaji kiwanda hicho.

Kunao waliohusishwa na kuangamia kwa muungano wa kumtetea mkulima MOCO, kunao wanaodaiwa kunyamazishwa katika vita dhidi ya waliopora kiwanda hicho, kunao waliohusishwa na skendo za uporaji na kuwatetea wanaokisiwa kukipora, kunao waliohusishwa na wizi wa chakavu za kiwanda hicho.

FCPA Fernandes Barasa

Kunao wanaokisiwa kufyonza ridhaa ya mkulima huku wengi wakihusishwa na hongo ya sukari na mishahara ghushi kutoka kwa kampuni hiyo. Hatua hizi zinakisiswa kuwa zilichangia pakubwa kufeli kwa kiwanda hicho kilichokua kitega uchumi kikuu magharibi mwa kenya kando na kutepeteza juhudi za kukifufua.

Kwa mujibu wa wataalamu wengi wa kiuchumi, ufufuzi wa kiwanda hicho unahitaji mkono wa serikali kando na uekezaji ili kuafiki lengo hilo ikizingatiwa kuwa kuna deni kubwa linalomkodolea macho mwekezaji.

Wanavyodadisi wachanganuzi wengi wa siasa, huenda mfumo wa ukabila unaosetiri siasa nchini ndio sababu ya kulegea kwa serikali kuu kuwajibikia ufufuzi wa kampuni hiyo na hivyo basi upo umuhimu wa serikali ya ugatuzi kuingilia kati na kufanikisha ufufuzi wa kiwanda hicho.

Fernandes Barasa (kushoto), Rais Uhuru Kenyatta (kati) na Naibu wa Rais William Ruto (kulia)

Huku wanasiasa wengi wakisakata denzi ya siasa za ugavana gatuzi la kakamga mwaka wa 2022, wakaaji wana kibarua kigumu kumchagua gavana atakayeekeza katika sekta ya viwanda kinyume na serikali ya sasa ya gatuzi hilo iliyoangazia sana sekta ya ujenzi.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya usambazaji umeme nchini (KETRACO) FCPA Fernandes Barasa, huenda ndiye wa kwanza na wa kipekee miongoni mwa wanaopania kumridhi Gavana Oparanya anayekumbatia sekta ya viwanda kama ajenda yake kuu katika uongozi.

Kwenye mazungumzo ya awali, Bw Barasa anasema kuwa kuekeza katika viwanda kutasuluhisha maswala tata katika ustawi wa jamii ikiwemo ajira ya dhamana kwa wakaaji, soko huru na bora kwa wanabiashara, malipo bora kwa wazalishaji wa mazao mbalimbali wakiwemo wakulima na kuvutia uekezaji Zaidi.

Kama njia mojawapo ya kurejesha mkono kwa jamii, waekezaji, kampuni na wanabiashara watajika hushiriki katika miradi ya kuboresha jamii ikiwemo kufadhili elimu, sekta ya afya, ujenzi wa barabara na ufadhili kwa wasiojiweza kakatika jamii.

Kwa mujibu wa mtaalamu huyu wa kiuchumi ambaye pia ni MwenyekitI wa taasisi ya uhasibu nchini ICPAK, kufufuliwa kwa kiwanda cha kusaga miwa cha mumias ni jambo la lazima kwa ustawi wa uchumi wa gatuzi la kakamega anaoelezea kuwa unategemea sana mishahara kustawi badala ya biashara.

Kufufuliwa kwa viwanda vilvyoangamia, kujenga viwanda vingine Zaidi na kuboresha hali ya viwanda vilivyopo ndio msingi wa ustawi wa uchumi ambapo Barasa anasema kuwa ni sharti wakulima na wafanyikazi wapate malipo mema ili kuwapa motisha ya kushiriki ipasavyo.

“Nina uhakika kuwa ntaboresha maslahi na malipo ya wafanyikazi na wakulima wa viwanda vya miwa kama Butali, West Kenya, Mumias Sugar n.k. Kunahitajika kiwanda cha majanichai Shinyalu, uchimbaji madini miongoni mwa mengine kando na majukumu mengine muhimu ya ugatuzi” alisema Bw Barasa.

Kabla ya kujiunga na KETRACO, utendakazi wa Barasa unadhihirika tangia mwaka wa 1997 alipoteuliwa kama naibu mhatibu katika shirika la ndege nchini (Kenya Airways) na baadae akateuliwa kama mkuu wa hazina na kiongozi wa akaunti za  viwanda katika shirikisho la ukusaji wa majani chai nchini (KTDA) mwaka 2002-2010.

Bw Barasa alijiunga na KETRACO Kama mkuu wa idara ya fedha, nafasi aliohudumu kwa miaka sita kabla ya kuchaguliwa kama meneja mkurugenzi mwaka 2015 wadhifa anaohudu hadi sasa.

Shirika la usambazaji umeme nchini KETRACO lilianzishwa 2/12 2008 na serikali ya kenya, na lengo la kukidhi mahitaji ya usambazaji umeme nchini kando na shirika la kenya power.

KETRACO ilinuia kuangazia usambazaji wa viwango vikuu vya stima,kukidhi mahitaji ya wateja wanaohitaji umeme kwa wingi yakiwemo mashirika na viwanda tajika nchini pamoja na uwiano wa umeme na baadhi ya mataifa kanda ya Africa mashariki na kati kama Tanzania, Ethiopia, Afrika Kusini, Uganda miongoni mwa mengine.

Hadi leo KETRACO imevunja historia kwa kuwa kampuni ya kwanza Afrika Mashariki na kati kuweka shughuli zake za ununuzi usambazaji na uuzaji kupitia mfumo wa kidijitali wa SAP. Kupitia KETRACO serikali imefadhili pakubwa usambazaji wa umeme chini yake meneja mkurugenzi wake FCPA Fernandes Barasa na mwenyekiti wake Mhandisi James Rege.

Tangia kuteuliwa kwake kama mkurugenzi, KETRACO imepunguza gharama ya umeme na kuingiza umeme kwa kampuni zilizokua zikitumia mafuta kama Kindaruma-Mwingi-Garissa miongoni mwa laini nyingine ambazo zinatumia umeme kwa viwango vikubwa.

Hatua hii imeletea serikali mabilioni ya pesa ambapo Garissa na Lamu pekee inazaa bilioni moja kila mwaka huku mradi wa 400kv Longarani-Suswa uliokamilika mwaka 2018 ukinusuru serikali takriban ya bilioni 8.5 ambazo zingetumika kwa mafuta.

Fernandes Barasa

Mradi mkuu wa Olkaria-Lesos-Kisumu Utahakikisha ustawi wa kawi magharibi mwa Kenya. KETRACO pia inanuia kuanzisha mradi wa 132kv Kisumu-Kakamega-Musaga utakaopunguza ukosefu wa umeme gatuzi la kakamega na kuvutia uekezaji na ustawi wa viwanda, hali ambayo itaongeza nafasi za ajira kwa vijana.

Barasa pia alihudumu kama Naibu Mwenyekiti wa Taasisi ya uhasibu nchini ICPAK na baadae akachaguliwa kama mwenyekiti wa taasisi hiyo nchini tangia mwaka 2015-2017 kando na kuwa yeye ni miongoni mwa wasomi 100 walioidhinishwa na taasisi hiyo kwa kitengo cha juu Zaidi cha ‘FCPA’.

Kando na KETRACO, Bw Barasa pia ni mfadhili wa kipekee wa Wakfu wa Barasa gatuzi la kakamega lenye malengo yakuimarisha hali ya maisha ya wakaaji.

Kupitia wakfu huu, ameweza kuimarisha vita dhidi ya saratani, kulipa karo kwa wasiojiweza, kufadhili makundi ya kina mama, kuimarisha vipawa katika jamii,ufadhili kwa makanisa na kununua pikipiki kwa makundi mbalimbali ya wanabodaboda.

Bw Barasa ambaye ni mzaliwa wa jamii ya wanga eneobunge la mumias mashariki na mkaaji wa eneobunge la Matungu, gatuzi la Kakamega alifuzu na Shahada ya Degree idara Fedha, Biashara na Umeneja, Chuo Kikuu cha Kenyatta na baadae akafuzu kiwango cha Uzamili na Uzamifu mtawalia.

Tajriba hii inamtafsiri kama aliye katika nafasi nzuri Zaidi kuimarisha uchumi na hali ya maisha ya wakaaji wa gatuzi hilo ikilinganishwa na wanaogombea kiti hicho.

RELATED ARTICLES

Most Popular

Recent Comments